Monday, 13 February 2012

CAMILLA AVUKA BODA HADI SUDAN KUSINI


Mwanadada anayekuja kwa kasi katika mziki wa kizazi kipya, kwa jina Camilla kutoka Malindi, ametoa wimbo mpya aliomshirikisha msanii kutoka Sudan Kusini anajulikana kama Saab Jay. Wimbo huo unajulikana Party East Africa unahusu mitindo ya kudensi na kuzungumzia maswala ya Afrika Mashariki.

"Nimeimba wimbo huu na kumshirikisha Saab jay ili kudumusha uana Afrika Mashariki na kupata flavour tofauti."

Msanii Camilla, pia ameimba vibao kama vile Super Star ambayo ilifanya vizuri hapa KETAU Express, Unanitatiza na Ni wewe. kwa sasa Camilla anapania kufanya collabo na msanii kutoka Tanzania ingawaje hajaiweka wazi kwa masela wake. Asema mwaka huu atajituma zaidi kimziki.

Wimbo Party East Africa umefanywa Ogopa Dj's ya humu nchini chini ya producer Antony.

No comments:

Post a Comment