Monday, 13 February 2012
BLOOM KUFANYA COLLABO TANZANIA
Wakati alipotoa kibao Msiachane, hakuwa amejulikana sana lakini baada ya kutoa wimbo Bye bye, ambacho alimshirikisha msanii Kizo B, msanii Mr. Bloom wa humu nchini, kwa sasa yuko nchini Tanzania kufanya collabo na wasanii Belle 9 na Shetta.
Safari hiyo ya Bloom, ambayo ilipamgwa na promoter Cal J, pia naye ni wa humu nchini, iliafikiwa hivi majuzi baada ya utafiti kufanywa na kuonekana kwamba Bloom alifaa kufanya collabo hiyo kutoka Tanzania na wasanii hao, chini ya producer Marko Chali aka Chali Mkali wa Tanzania.KETAU Express inamtakia Bloom kazi njema akiwa Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment