
Wanamuziki toka Goodlyf, Radio na Weasel waliogonga vichwa vya muziki kwa wimbo wao Potential na Talk n Talk na kuwa na beef kali na msanii analiyenoga Chameleone na Bebe cool.
Udashdash unaotufikia ni kuwa beef kali imeibua kati ya wasanii hawa na chipukizi Eddie Kenzo anayevuma kwa vibao Stamina na Bolingo. Ubishi huu unafaamika kuanza mwaka jana baada ya Kenzo kudinda kufanya collabo na wawili hao, huku Kenzo akisema alikuwa na shughuli nyingi.
Ubishi ulianza na Radio na Weasel waliamua kununua haki miliki ya wimbo uliovuma Abakyala babeeyi ambayo awali ilinunuliwa na Kenzo. Wawili hao walisemekana kulipa Ugsh 1,000,000 sawa na Ksh 35,000 kwa haki miliki ya wimbo huo. Kutonesha kidonda zaidi, walimnunua msanii chipukizi Booerman kufanya remix mojawapo ya myimbo mpya ya Kenzo ilikumtia lawama.

No comments:
Post a Comment