![]() |
| AMINI |
Msanii huyu anakwenda kwa jina la Amini Mwinyimkuu ‘Amini’ aliyekuwa kwa kundi la THT. Inafaamika kwamba
msela huyu huenda akatimuliwa ndani ya kundi hilo kutokana na utovu
wa nidhamu.
Akiongea Amini alisema kikubwa kinachotaka
kumfukuzisha hapo ni kuchukia tabia za baadhi ya wasanii wa kundi hilo
ambao wanajipendekeza kwa mabosi. Msanii huyu alisema si kweli kuwa ana nidhamu mbovu kama
inavyodaiwa lakini kutokana na hulka yake ya kupenda kusimamia ukweli
kwenye kila jambo basi amekuwa akionekana mkorofi.
Mpaka anaongelea swala hili uongozi wa THT ulikuwa unataka kukaa kikao kumjadili kwamba afukuzwe au abaki.“Yani nimesikia kwamba najadiliwa na uongozi wa kundi ili niweze
kufukuzwa lakini kwa upande wangu sioni kama ni tatizo kwa sababu kama
kipaji ninacho hivyo nasema kama mimi ni mtovu wa ni nidhamu sawa niko
tayari kuondoka,” alisema.

No comments:
Post a Comment